MASUPASTAA ambao ni wachumba (wanasema wenyewe), Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakiwa
katika pozi la kimahaba kitandani Naf beach hotel. Picha hizi Wema
amezitupia katika akaunti yake ya Instagram na kuandika maneno
yafuatayo "Thank
God tumemaliza salama...Nd we are Happy it went
well...Alahamdulillah....Baadae inshallah...Tulale kwanza alafu yale
mapichapicha na kila kitu, leteeeeers..
Featured Posts
Monday, May 5, 2014
TAZAMA PICHA JINSI WEMA SEPETU NA DIAMOND WALIVYOFUNIKA NDANI YA MTWARA
Diamond doing what he does best
Madam on point reppin' big time
This was Mtwara next stop........... stay tuned
Wasafi Classic Dancers doing what they do best
Friday, May 2, 2014
HII NDIO HOTEL YA KISASA ILIYOPO MTWARA AMBAYO DIAMOND ANAFANYA SHOW YAKE LEO,ITAZAME HAPA
.Ni moja ya hotel
bora kabisa Kusini mwa Tanzania na Tanzania kwa
ujumla..ikiwa located pembezoni kabisa
mwa ufukwe wa bahari ya hindi
.. mbali ya vyumba bora,chakula na huduma safi zinazopatikana
pale utaweza kufurahia hewa safi na manzali ya kuvutia ya
Ufukwe wa bahari ..Wiki hii team nzima ya
Wasafi Watakuwa hapa.
MWONEKANO WA NJE,USIKU
BAR
CHUMBA CHA MIKUTANO
SITTING ROOM YA MOJA YA VYUMBA
MOJA WAPO YA VYUMBA
Wednesday, April 30, 2014
DIAMOND PLATINUMZ AWAAMBIA WAKAZI WA MTWARA WASIKOSE SHOW YAKE YA IJUMAA KWANI ANAKUJA NA SUPRISE BABKUBWAAA
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa (kulia)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na udhamini wa Tamasha la Heels & Ties litakalofanyika makonde beach Mtwara na kutumbwizwa na Msanii mahiri Diamond Platinum na Wema Sepetu. Mteja anaweza kununua tiketi yake kwa njia ya M-pesa kwa kutuma pesa kwenda 0754 980 769 na kupata punguzo la asilimia 20%. Pamoja nae katika picha ni Nassib Abdul Maarufu Kama Daimond Platinum.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul, Diamond Platinum akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na Tamasha la Heels & Ties litakalofanyika makonde beach Mtwara na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, Wateja wanaweza kununua tiketi yake kwa njia ya M-pesa kwa kutuma pesa kwenda namba 0754 980 769. na kupata punguzo la asilimia 20%. Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa
Nyota wa muziki wa Bongo flava nchini anayepasua anga ya Afrika, Rais wa wasafi kama wengi wanavyomuita, Diamond Platnum, Dangote ameahidi makubwa kwa mashabiki wake wote wa Mkoa wa Mtwara kuhusu show ya aina yake inayotarajiwa kufanyika katika umbi wa Makonde Club mjini Mtwara siku ya ijumaa tarehe 2 mwezi huu.
Msanii huyo aliyeafanikiwa kujizolea mamilioni ya mashabiki wa muziki wa Bongo flava atasindikizwa na kipenzi chake, Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu - 'Beautiful Onyinye' au Madame kama mashabiki wake wanavyopenda kumwita.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katika ofisi za Vodacom Tanzania, ambao ndio wadhamini wa tamasha hilo amesema Mashabiki wakae mkao wa kula burudani ya nguvu ya muziki kutoka kwa kipenzi chao ambaye hafikirii kukosea wala kuwaangusha mashabiki wake katika show zake zote anazozifanya.
"Mashabiki wote waliopo Mtwara watashuhudia nikiimba live nyimbo yangu mpya ya My number One remix niliyomshirikisha Davido kutoka nchini Nigeria. Kwa kawaida huwa sipendi kuwaangusha mashabiki zangu hivyo basi nawaahidi makubwa sana katika tamasha hilo na ningependa kuwaona wengi wakihudhuria show hiyo kwani kutakuwepo na mengi ambayo hawakutarajia kuyaona" Alisema Diamond.
Msanii Diamond ambaye kwa sasa ndiyo mwenye mafanikio makubwa ya kimuziki nchini amekuwa ni kivutio kikubwa kwa mashabaiki wa ndani na nje ya nchi kila mahali anapoalikwa kufanya shoo na hivyo kujizolea sifa lukuki na hata kuchaguliwa kuwania tuzo mbali mbali za muziki barani Afrika.
Kwa upande wao wadhamini wa tamasha hilo Mkuu wa kitengo cha masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amesema mtandao wao unajivunia kudhamini tamasha kubwa kama hili kwani hakuna kitu ambacho wanakijali kama wateja wao haijalishi wapo kona gani ya Tanzania.
"Tunajivunia kuwa sehemu ya Wadhamini wa Tamasha hili kubwa, Vodacom siku zote tumekuwa tukitoa kipaumbele kwa wateja wetu, Kipindi cha Pasaka tulifanya Tamasha pale coco beach na sasa ni zamu ya watu wa Mtwara" alisema Twissa na kuongeza.
"Tutawafikia wateja wetu popote pale walipo na kuwapa burudani Vodacom imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwa kipindi chote hicho watanzania wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya tuwe mtandao unaaongoza siku zote Hivyo hatuna budi kuwafanyia yale ambayo wanaweza wakafurahi ikiwemo kuwaletea burudani kama hii".
"Ili kuwarahisishia wateja wetu na wananchi kwa ujumla, mteja anaweza kununua tiketi yake kwa njia ya M-pesa kwa kutuma pesa kwenda 0754 980 769. Na atapatiwa ufafanuzi wa jinsi ya kupata tiketi yake. Wateja watakaotumia njia hii watapata punguzo la asilimia 20 (20%). Wateja wa Vodacom na Mashabiki wote kwa ujumla wasiache kuhudhuria shoo hiyo ambayo itakuwa na kishindo kikubwa na kwa aina yake". Alisema.
Aidha, "Vodacom tunaahidi kuenedelea kuwaunga mkono wasanii wetu wa Kitanzania na kujivunia kilicho chetu, wote ni mashahidi kwa namna ambavyo tumekuwa msitari wa mbele kuwaunga mkono wasanii wetu na tutaendelea na jitihada hizo na kufikia viwango vya wasanii wengine wa kimataifa," Alihitimisha Twissa.
Tuesday, April 29, 2014
FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi
Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani
Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.
Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.
Sunday, April 27, 2014
DIAMOND NA WEMA KUHAMIA MTWARA
DAR ES SALAAM Aprili 27, 2014 … Wakazi wa kusini mwa
Tanzania yaani mkoa wa Mtwara wametakiwa kukaa mkao wa kula burudani ya
nguvu ya muziki itapigwa moja kwa moja jukwaani siku ya tarehe 2 ya
mwezi wa Mei katika ukumbi wa Makonde Club.
Shoo hiyo ya kipekee na ya aina yake italetwa na si mwingine bali ni mkali wa muziki wa bongo flava nchini anayepasua anga ya Afrika ya Mashariki kwa sasa kupitia vibao vyake vitamu kama vile cha My Number One remix alichomshirikisha msanii Davido kutoka nchini Nigeria, Raisi wa wasafi ama Diamond Platinumz”Asali ya warembo” kama mashabiki wake wanavyomwita.
Mwanamuziki Diamond atafanya shoo laivu mkoani Mtwara chini ya udhamini mkubwa wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania akisindikizwa na kipenzi chake, Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu – ‘Beautiful Onyinye’ au Madame kama mashabiki wake wanavyopenda kumwita.
Msanii Diamond ambaye kwa sasa ndiyo mwenye mafanikio makubwa ya kimuziki nchini amekuwa ni kivutio kikubwa kwa mashabiki wa ndani na nje ya nchi kila mahali anapoalikwa kufanya shoo na hivyo kujizolea sifa lukuki na hata kuchaguliwa kuwania tuzo mbalimbali za muziki barani Afrika.
Akizungumzia juu ya shoo hiyo ya kukata na shoka kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amebainisha kuwa tukio hili limeandaliwa ikiwa ni sehemu ya burudani kwa wateja wetu, kufurahi kwa pamoja na kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma zetu.
“Hakuna kitu ambacho tunajali na kukithamini kama wateja wetu, haijalishi wawe kona gani ya Tanzania, walipo popote tutawafikia. Vodacom imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwa kipindi chote hicho watanzania wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya tuwe mtandao unaaongoza kwa mawasiliano nchini.” Alisema Twissa.
Kwa kuongezea Twissa amewataka wakazi na mashabiki wote wa Diamond na muziki wa Bongo Flava kujitokeza kwa wingi kwani mbali na burudani kutakuwepo na huduma na bidhaa mbali mbali za Vodacom.
Katika kunogesha shoo hiyo kwa wakazi wa kusini Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu naye akasema haitokuwa poa kama asipomsindikiza asali wake wa moyo kwenda kujivinjari pande hizo na mashabiki wao. Kwa tafsiri nyingine mashabiki wa Mtwara wanabahati kubwa ya kutembelewa na mastaa wawili wakubwa kutoka tasnia mbili tofauti nchini.
“Hii shoo si ya kukosa kabisa kwani hakuna kiingilio bali ni uwepo wako tu na kujiandaa kwako kwa burudani ndio kinachohitajika. Tunawapenda sana wateja wetu wa Mtwara, hatuna uwezo wa kulipa kutokana na kuwa wateja wetu waaminifu siku zote lakini ninaamini kwa pamoja tunaweza kujumuika na kufurahia wakati tulionao. Naombeni mjitokeze kwa wingi, rafiki amlete rafiki yake ili tuwe pamoja siku hiyo.” Alimalizia Twissa

Subscribe to:
Posts (Atom)